Mganda wa Coastal Union hali tete

DESEMBA 12,2022 Katibu Mkuu wa Coastal Union, Omar A.S Ayoub alimtambulisha kocha Yusuf Chipo kuwa kocha mkuu wa timu hiyo.

Chipo alisaini mkataba wa mwaka mmoja wa kuinoa timu hiyo ambapo alichukua mikoba ya Juma Mgunda anayeinoa Simba.

Taarifa zinaeleza kuwa kocha huyo kwa sasa yupo kwenye mazungumzo na mabosi wa timu hiyo ili aweze kuvunja mkataba wake.

Mganda wa Coastal Union hali tete

Sababu kubwa ya kuwa kwenye hesabu za kuondolewa hapo ni mwendo mbovu wa timu hiyo na mchezo uliopita alishuhudia akipoteza kwa kufungwa bao 1-0 dhidi ya KMC.

Kete inayofuata ni dhidi ya Yanga, Uwanja wa Mkapa, Desemba 20,2022.

Acha ujumbe