Baada ya leo kuuchezea  kichapo dabi yake ya pili dhidi  Azam,  huku akitoa sare kwenye Kariakoo dabi dhidi ya Yanga, kocha wa Simba Juma Ramadhan Mgunda amesema kuwa kazi yake iliyomleta kwenye klabu hiyo bado haijamalizika.

Mgunda alisema viongozi wa Simba walimuamini kuwa anaweza akaifikisha sehemu timu hiyo na licha ya kuwa tayari ameshaingia kwenye mioyo ya wanasimba wengi, lakini yeye anaona bado ana mlima mrefu wa kupanda ili kufika kileleni.

mgunda

Mgunda alisema, ligi bado mbichi, ligi ya mabingwa ndiyo kwanza nayo imeanza kuwa ngumu na bado kuna mashindano mengine yanakuja mbele na anatakiwa kuyavuka na kuiweka timu hiyo kwenye sehemu nzuri ambayo inatakiwa kuwa.

“Kazi bado haijaanza, kwangu mimi kama mwalimu naona bado sijafika pale ambapo timu inatakiwa ifike. Najua mashabiki wana upendo mkubwa kwangu na wanaridhika na nifanyacho na ninawashukuru sana.

“Lakini niwaambie kazi hii ngumu sana na bado kuna jukumu kubwa mbele yetu. Ligi ndiyo kwanza mbichi, kuna mashindano mengine mbele ya ndani na kubwa bado tupo ligi ya mabingwa. Bado tunatakiwa tufanye kazi sana,” alisema.

Mgunda ameiongoza Simba kwenye mechi saba, akishinda mechi sita na kutoka sare katika mechi moja ambayo ni dhidi ya Yanga na jana Alhamisi aliongoza Simba kwenye mechi ya nane dhidi ya Azam FC.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa