MGUNDA, MATOLA WAIPIGIA HESABU KALI DODOMA JIJI

BENCHI la ufundi la Simba likiongozwa na kocha Juma Mgunda na Suleiman MatolaΒ  limebainisha kuwa maandalizi yanaanza kuelekea mchezo wao ujao dhidi ya Dodoma Jiji unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Jamhuri, Dodoma.

Ipo wazi kwamba mchezo huo awali ulipangwa kuchezwa Mei 16 2024 lakini umepangiwa tarehe mpya ambayo itakuwa ni Mei 17 2024.mgundaMchezo uliopita Simba chini ya Juma Mgunda akishirikiana na Seleman Matola iligawana pointi mojamoja na Kagera Sugar kwa kushuhudia ubao wa Uwanja wa Kaitaba ukisoma Kagera Sugar 1-1 Simba.
Bao la Simba lilifungwa na Ladack Chasambi na lile la Kagera Sugar lilifungwa na Obrey Chirwa.

Mgunda amesema; β€œMakosa ambayo yamepita tunyafanyia kazi kwa ajili ya kuona kwamba mechi zijazo tunapata matokeo mazuri, kikubwa ni kuona kila mchezaji anatimiza majukumu yake.mgundaβ€œWachezaji wapo tayari na ni muda wa kupambana kufanya vizuri kwenye mechi zetu zilizobaki kwa kuwa hakuna mchezaji ambaye hapendi kufunga.”

Simba ipo nafasi ya tatu kwenye msimamo ina pointi 57 inakutana na Dodoma Jiji iliyo nafasi ya 11 na pointi 30.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.