MGUNDA MFALME DABI YA MZIZIMA

KOCHA wa muda ndani ya Simba SC Juma Mgunda, alimaliza mchezo wa Dabi ya Mzizma dhidi ya Azam FC akiwa Mfalme na Boli likitembea kweli kweli.

Azam FC wamepoteza pointi tatu mbele ya Simba katika mchezo wa mzunguko wa pili uliokuwa na ushindani mkubwa, ukipigwa Benjamin Mkapa, Jana.

Baada ya dakika 90 ubao wa Uwanja wa Mkapa ukasoma Azam FC 0-3 Simba jambo ambalo limeonekana kuwashtua wengi, Kwani watu wengi hawakua wanawapa nafasi vijana wa kocha Juma Mgunda lakini wakafanikiwa kuwashangaza wengi ambao hawakuwapa imani.mgundaNi Sadio Kanoute aliyewapa uongozi vijana wa kocha Mgunda akipachika bao la ufunguzi dakika ya 63 kamba ya pili ni Fabrice Ngoma dakika ya 77 na ile ya tatu ni Duchu dakika ya 89.
Azam FC walikuwa na nafasi yakufunga kipindi cha kwanza walikosa penalti kupitia kwa Feisal Salum aliyegongesha mwamba kipindi cha kwanza.mgundaKatika mchezo wa mzunguko wa kwanza ubao ulisoma Simba 1-1 Azam FC lakini jana matokeo yamekua ya tofauti baada ya Mnyama kutoka kusipojulikana na kupata ushindi wa mabao matatu kwa bila mbele ya Azam Fc.

Acha ujumbe