Mgunda: Tunahitaji Alama Tatu Muhimu

Kocha mkuu wa klabu ya Simba Juma Mgunda ameongea na wanahabari leo hii kuelekea mchezo wao dhidi ya klabu Polisi Tanzania na kueleza mipango yake kuelekea mchezo huo ni kupata alama tatu muhimu katika mchezo huo.

Kocha huyo anaeleza “Maandalizi ya mchezo yamekamilika na wachezaji wapo kwenye hali nzuri,Tunajua mechi itakua ngumu. Na Polisi haipo kwenye nafasi nzuri tutaiheshimu lakini malengo yetu ni kupata alama tatu. Klabu ya Simba itahitaji kupata matokeo mazuri katika mchezo huo ili iweze kukaa kileleni kwa mwa msimamo.mgundaMchezo wa Simba na Polisi Tanzania ambao unatarajiwa kupigwa katika dimba la Ushirika mkoani Kilimanjaro hapo kesho majira ya saa kumi kamili jioni. Klabu ya Polisi Tanzania haipo kwenye kiwango kizuri kwasasa hivo nao wanatarajia kutoa ushindani mkali hapo kesho ili waweze kujinasua kwenye nafasi ya 15 na alama zao 9 tu.

Simba wao wametoka kudondosha alama dhidi ya Mbeya City mchezo uliomalizika huko jijini Mbeya hivo watakua wanahitaji alama tatu muhimu ili kuendelea kujiweka kwenye mazingira mazuri ya kugombania Ubingwa wa ligi kuu ya NBC msimu huu baada ya kuukosa msimu uliomalizka.mgundaSwali ambalo wadau wanaendelea kujiuliza je Simba wataendelea na rekodi yao mbovu ya kuteseka katika viwanja vya mkoani kwani msimu huu wakiwa wamefanikiwa kupata alama tatu tu kwenye viwanja vya mkoani.

SIMBA

Je wewe hucheza Kasino Mtandaoni na umekuwa ukijiuliza ni mchezo gani rahisi na mzuri kwa ushindi? Basi Usihangaike Aviator ni rahisi zaidi kucheza na kushinda, kingine cha zaidi ni kwamba Aviator Bonanza imerudi tena Cheza zaidi ujiweke kwenye nafasi ya kushinda Samsung A23.

BONYEZA HAPA KUCHEZA

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.