Kocha mkuu wa klabu ya Simba Juma Mgunda amesema wanakwenda kucheza mchezo wa kesho dhidi ya klabu ya Azam huku wakiwaheshimu klabu hiyo, Lakini watahitaji alama tatu katika mchezo huo.mgundaKocha Mgunda amezungumza kua mchezo wa derby ulishamalizika hivo mchezo unaofuata ni dhidi ya Azam, Na walijua baada ya kumaliza mchezo wa derby mchezo ambao ungefata ni dhidi ya wanalambalamba na kuhusu hilo wameshajiandaa.

Kocha huyo ambaye ameiongoza timu katika mechi 9 huku 7 zikiwa za kimashindano na hajapoteza mchezo hata mmoja, hivo kuelekea mchezo wa Azam watu wana hamu ya kuona kocha kama ataendeleza rekodi yake kutopoteza mchezo mbele ya matajiri hao wa Dar-es-salaam.mgundaPia Mgunda ameeleza wachezaji ambao watakosekana katika mchezo huo wa kesho ni Israel Mwenda aliepata majeraha atakaa nje kwa wiki mbili, Kanoute ambae anaendelea kuugua, pamoja na Mzamiru Yassin ambae ataukosa mchezo kutokana na kanuni baada ya kupata kadi tatu za njano.

 

 

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa