MICHO: Jana wakati mchezo wa watani wa jadi Yanga dhidi ya Simba ulipokuwa ukiendelea, ulishuhudia watu wengi kutoka nchi tofauti wakihudhuria uwanjani kushuhudia mchezo huo wa historia.
Miongoni mwa watu maarufu waliojitokeza jana, ni kocha wa timu ya taifa ya Uganda Milutin ‘Micho’ alionekana kwenye mchezo wa Derby na kuzua maswali mengi kuwa huenda akachukua nafasi ya kocha wa Yanga Nasreddine Nabi
Mapema hii Leo ameweka wazi kuwa bado yeye ni kocha wa Uganda na hakuna habari zozote za yeye kuhitajika na timu yeyote kutoka Tanzania.
βHapana. Mimi Bado ni kocha wa Uganda na ninafanya kazi yangu.β – Alisema Micho
Siku za nyuma pia aliwahi kuja nchini aliyekuwa kocha wa zamani wa mabingwa wa Ligi ya mabingwa barani Afrika CAFCL Al Ahly ya Misri Pitso Mosimane, ambaye alikuja kwa mualiko maalum wa klabu ya Yanga kuelekea kwenye kilele cha wiki ya mwananchi mwaka huu 2022. Wengi waliwaza huenda akachukua nafasi ya kocha Nabi ambaye alisemekana mkataba wake umemalizika klabuni hapo.