Kocha wa Timu ya Taifa ya Uganda, raia wa Serbia Milutin Micho ambaye aliwahi kuinoa Yanga miaka ya nyuma amefunguka kuwa kwa hapa Tanzania klabu na uongozi wa Yanga ni kama ndugu zake na ni kawaida kwake kuja hapa kuwatembelea siyo jambo ngeni.

Micho alisema, wakati yupo Tanzania akifanya kazi ya ukocha aliishi vizuri na viongozi wa Yanga ingawa aliondoka kwenye kipindi ambacho bado alikuwa anahitaji kufanya makubwa kwenye timu hiyo, haiwezi kuondoa ukweli kuwa yeye ni mwanafamilia wa Yanga.

Yanga, Micho: Yanga ni Familia Yangu Kabisa, Meridianbet

“Yanga ni familia yangu, siyo jambo la ajabu mimi kuja hapa na kuonana na ndugu zangu. Niliishi hapa kwa uzuri ingawa haikuwa kwa kipindi kirefu lakini ulikuwa wakati mzuri sana,”

alisema.

Micho aliwahi kuinoa Yanga mwaka 2007 lakini akaja kutimuliwa baada ya timu hiyo kufungwa kwa penalty na Simba baada ya sare ya 1-1.

Kwenye mchezo uliochezwa kwenye uwanja wa Jamhuri Morogoro ambao ulitumika pia kubadili kalenda ya Ligi Kuu Bara kutoka kuchezwa Januari na Kwenda Agosti.

Wikiendi iliyopita alikuwepo Dar kutazama dabi ya Kariakoo Simba na Yanga na kisha alikaribishwa kwenye ofisi ya rais wa Yanga Eng. Hersi Said na kukabidhiwa jezi za timu hiyo.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa