Kocha Mkuu wa Geita Gold, Felix Minziro amefunguka kuwa nyota wao anayehusishwa kutakiwa na klabu mbalimbali, Saido Ntibazonkiza tayari alishaongeza mkataba.

Tayari dirisha dogo la usajili lilifunguliwa Desemba 15 mwaka huu na Shirikisho la Soka nchini (TFF) kwa ajili ya timu mbalimbali kuongeza nguvu kwenye vikosi vyao.

Ntibazonkiza ambaye alijiunga na Geita Gold kwenye dirisha kubwa la usajili amefanikiwa kuonyesha kiwango kizuri akiwa na kikosi hicho.

Minziro aweka wazi mkataba wa Saido Geita Gold

 

Akizungumzia tetesi hizo, Minziro amesema “Ni kweli hata mimi nimezisikia tetesi hizo na Geita Gold tuna wachezaji wengi hivyo haitupi shida.

“Nakumbuka ni juzi tu Saido alisaini mkataba mpya hivyo sijajua hilo viongozi wanalichukuliaje lakini hata mimi nimeona kwenye mitandao kwamba watu wa Simba na baadhi ya timu wanahitaji saini yake.”

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa