Kocha Mkuu wa Yanga Miguel Gamondi amesema bado kazi haijaisha kwenye mechi za kimataifa hivyo wataendelea kufanya maandalizi kuwa imara kwa mechi zinazofuata.
Yanga ni timu ya kwanza kwenye ardhi ya Tanzania kutinga hatua ya robo fainali ikiwa na mchezo mmoja mkononi huku watani zao wa jadi Simba wakiwa na kibarua Machi 2 kutambua hatma yao kutinga hatua ya robo fainali ama kugotea katika hatua ya makundi.Mchezo wa mwisho kwa Yanga atika hatua ya makundi ni dhidi ya Al Ahly ya Misri unaotarajiwa kuchezwa Machi Mosi 2024.
Yanga ipo nafasi ya pili kwenye kundi D vinara ni AL Ahly wenye pointi 9, Yanga ni pointi 8 wakiwa wamecheza mechi tano.
Kocha Gamondi amesema: “Kazi kubwa ya kupata ushindi ni muhimu kwenye mechi ambazo tunacheza ili kuongeza hali ya kujiamini kwa kuwa kila mchezaji yupo tayari kuona tunaendelea kuwa kwenye ubora.“Kila mmoja anapenda kuona wachezaji wanapata matokeo na uzuri ni kwamba wachezaji wanajituma na kutimiza majukumu yao kwenye mechi ambazo tunacheza hivyo bado tuna kazi ya kufanya,” amesema Gamondi