BAADA ya kutambulishwa ndani ya kikosi cha Simba kiungo wa kazi ngumu uwanjani Luis Miquissone amepewa masharti mazito yatakayomrejesha kwenye ubora wake.
Luis aliwahi kuitumikia Klabu ya Simba Januari 2020 hadi Agosti 2021 alipoibukia ndani ya Al Ahly alitambulishwa kwa mara nyingine Julai 22 ndani ya Simba.Clatous Chama kiungo wa Simba amesema kuwa alikuwa anawasiliana na Miquisonne mara nyingi kuhusu masuala ya mpira hivyo kurejea kwake ni furaha na lazima apambane ili awe bora ikiwa ni miongoni mwa masharti mazito kufikia mafanikio.
“Ninamuomba Mungu apambane na azidi kujituma kuwa bora kwa kuwa kwenye maisha ya mpira ukiwa sehemu na haupati nafasi ya kucheza kuna vitu ambavyo vinakosekana hivyo kurudi kwake ni furaha.”
Timu ya Simba imewea kambi Uturuki kwa ajili ya maandalizi ya msimu wa 2023/24 ikumbukwe kwamba mara ya mwisho kutwaa mataji ilikuwa ni 2021 msimu alioondoka Miquisonne.Kurejea kwake ni kazi nyingine kupambania rekodi za kutwaa Ngao ya Jamii, Kombe la Azam Sports Federation na Ligi Kuu Bara ambayo yote kwa msimu wa 2022/23 yalikwenda kwa Yanga.
Katika anga la kimataifa kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika ni hatua ya robo fainali waligotea hivyo hesabu itakuwa kufika mbali hatua ya nusu fainali mpaka fainali.