Aliyekuwa mchezaji wa zamani wa Simba, na Geita Gold Miraji Athumani amesajiliwa na klabu ya JKT Tanzania inayoshiriki ligi daraja la kwanza mpaka mwisho wa msimu huu.

 

Miraji Athumani( Sheva) Aibukia JKT Tanzania

Miraji Athumani alicheza Simba na kubeba mataji mbalimbali iliwemo Ligi Kuu Kombe la Azam na mengine mengi kabla ya kuhamia kwa wachimba madini wa Geita, Geita Gold ya Felix Minziro.

Baada ya kwenda huko kwa wachimba madini mchezaji huyo amekuwa hapati nafasi mara kwa mara ya kucheza kutokana na kikosi ambacho Minziro anacho na hivyo ni bora kuona akatafute changamoto sehemu nyingine.

Miraji Athumani( Sheva) Aibukia JKT Tanzania

JKT Tanzania ambao msimu juzi walishuka daraja kutokana na kuwa na kiwango kibovu na licha ya kujitahidi msimu uliopita kuwa katika nafsi nzuri kwenye ligi yao bado walishindwa kupanda daraja baada ya kupoteza mechi yao waliyocheza dhidi ya Prisons.

Hivyo kusajiliwa kwake kwenda timu hiyo inaweza kuwasaidia JKT kufanya vizuri tena msimu huu na kupanda daraja moja kwa moja bila kucheza play off, kwani timu za ligi kuu zina uzoefu mkubwa kulinganisha na ligi ya kwanza.

 

 

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa