Kiungo wa muda mrefu ndani ya klabu ya Simba Jonas Mkude amekua akiacha maswali mara kwa mara kwasasa kwa mashabiki wa klabu ya Simba juu ya muenendo wake ndani ya klabu ya Simba.

Kiungo Jonas Mkude amekua mguu nje mguu ndani ndani ya klabu ya Simba kutokana na kutokuhusika kwenye michezo kadhaa ya klabu hiyo, Kiungo huyo leo hajajumuishwa kwenye kikosi ambacho kitasafiri kuelekea nchini Uganda kucheza na Vipers mchezo wa ligi ya mabingwa ulaya.mkudeKiungo huyo mkongwe ndani ya timu hiyo inaelezezwa amekua hayupo sawa na uongozi ndani ya timu hiyo kwani amekua hajumuishwi kwenye michezo kadhaa ndani ya klabu hiyo, Taarifa mbalimbali zinaeleza kua mchezaji huyo amekua haumwi lakini hajumuishwi kwenye kikosi cha timu hiyo.

Kiungo Mkude alionekana mara ya mwisho katika mchezo dhidi ya Raja Casablanca akitokea benchi ambapo klabu hiyo ilipoteza kwa mabao matatu kwa bila, Lakini vilevile mchezaji huyo pia alishakosekana katika michezo kadhaa iliyopita ndani ya timu hiyo kabla ya mchezo dhidi ya Raja Casablanca.mkudeJonas Mkude hakua sehemu ya kikosi katika mchezo wa ligi kuu ya NBC dhidi ya klabu ya Azam Fc, Lakini vilevile leo pia amekua sio sehemu ya kikosi ambacho kitasafiri kuelekea nchini Uganda kumenyana na Vipers katika mchezo wa hatua ya makundi kigi ya mabingwa Afrika kutokana na hali hii inafanya wadau wa soka na mashabiki wa kalbu hiyo kuendelea kujiuliza maswali mengi juu ya hatma ya mchezaji huyo klabuni hapo.

 JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa