Mkude Kupewa Thank You Yanga

Taarifa zinaeleza kua kiungo wa zamani wa klabu ya Simba Jonas Mkude huenda akapewa mkono wa kwaheri ndani ya klabu ya Yanga baada ya mkataba wake kumalizika ndani ya timu hiyo.

Kiungo Mkude alipewa mkataba wa mwaka mmoja ndani ya klabu ya Yanga na umemalizika huku klabu hiyo ikielezwa haina mpango wa kumuongeza kandarasi mpya, Hivo jambo lililobaki ni moja tu kupewa mkono wa kwaheri ndani ya viunga vya Jangwani.MkudeKiungo huyo ambaye alijiunga na mabingwa hao wa ligi kuu ya NBC akitokea klabu ya Simba amekua hana msimu bora sana ndani ya kikosi cha Yanga, Kwani amekua hapati nafasi ya kucheza mara kwa mara hivo klabu hiyo inaelezwa kufikia uamuzi wa kuachana nae.

Mkude atakumbukwa zaidi ndani ya klabu ya Yanga kupitia mchezo wa robo fainali ya ligi ya mabingwa Afrika dhidi ya Mamelodi Sundowns, Ambapo alionesha kiwango bora sana katika michezo yote miwili kuanzia mchezo wa kwanza hapa Tanzania na mchezo marudiano kule Afrika Kusini.

Acha ujumbe