MO Awapongeza Simba Queens

MWEKEZAJI na Rais wa Heshima wa klabu ya Simba SC Mohammed Dewji ‘MO’ ametumia mtandao wake wa kijamii kutuma pongezi kwa timu ya wanawake ya Simba Queens kufuzu hatua ya nusu fainali ya Michuano ya Klabu bingwa kwa wanawake barani Afrika.

 

MO Awapongeza Simba Queens

Kwenye ukurasa wa Twitter wa Tajiri huyo alidhihirisha hisia zake kwa timu hiyo baada ya kufuzu hatua ya nusu fainali na kuandika kuwa ‘mmetufanya tujivunie sana’

“Hongereni sana @simbaqueensctz kwa kufanikiwa kufika Nusu fainali ya Ligi ya Wanawake ya Mabingwa Afrika, kwa mara ya kwanza katika Historia! Umetufanya tujivunie sana. Nusu fainali tunakuja! #NguvuMoja #CAFWCL”

 

Simba Queens Kucheza na Mamelod Sundowns Nusu Fainali

Sasa Timu hiyo kutoka Tanzania itakutana na Miamba ya Afrika Kusini ambao pia ni Mabingwa watetezi Mamelod Sundowns kwenye hatua hiyo, huku AS FAR watakutana na TP Mazembe ya DR Congo. Mshindi wa jumla ataenda kucheza fainali hizo ambazo kwa upande wa Simba Queens huenda wakazidi kuandika rekodi mpya na nzuri kwenye michuano hiyo ambayo wameshiriki kwa mara ya kwanza mwaka huu.

Acha ujumbe