Mwekezaji na Rais wa heshima wa klabu ya soka ya Simba Mo Dewji amekitembelea kikosi cha klabu hiyo kilichoweka kambi fupi nchini Dubai mapema leo hii.
Klabu ya Simba imeweka kambi fupi ya siku saba nchini Dubai ambapo watakua wakifanya mazoezi kwajili ya kujiandaa na michuano mbalimbali inayowakabili. Klabu hiyo ilitoka nchini Trehe 7 mwezi huu wa Januari na kuelekea nchini Dubai.Mwekezaji wa klabu hiyo Mo Dewji amekitembelea kikosi cha Simba kilichoweka kambi nchini Dubai na kuzungumza na wachezaji wa klabu hiyo mambo mbalimbali, Mojawapo ni kuhakikisha wanafanya maandalizi makubwa ili timu hiyo kutwaa taji la ligi ya mabingwa Afrika.
Mwekezaji huyo amekua na utaratibu wa kuongea na wachezaji wa Simba kila atakapokua anapata nafasi ya kukutana na wachzaji hao, Ikumbukwe pia kua Mo deji ndio alipendekeza kua klabu hiyo inapaswa kuweka kambi fupi nchini Dubai kabla ya kurudi kwenye michuano mbalimbali ambayo klabu hiyo inashiriki.Taarifa zinaeleza pia kua mwekezaji Mo Dewji alihakikisha kua klabu ya Simba inaweka kambi nchini Dubai ili kuipa timu hiyo kufanya mazoezi vizuri chini ya mwalimu mpya klabuni hapo, Klabu ya Simba imetambulisha kocha mpya siku kadhaa zilizopita Mbrazil Roberto Oliviera.