Morrison Atoa Neno Baada ya Penati ya Utata

Kiungo mshambuliaji wa Yanga SC Bernard Morrison ambaye aliifungia timu yake goli la penati lililoipatia alama tatu muhimu dhidi ya Geita Gold kwenye dimba la CCM Kirumba Jijini Mwanza, ametolewa ufafanuzi kuhusu tukio la utata la penati baada ya mchezaji wa Geita kuamuliwa kuushika mpira akiwa nje ya 18 na mwamuzi kuamua mkwaju wa penati.

 

Morrison Atoa Neno Baada ya Penati ya Utata

Kutokana na maamuzi hayo yaliyoipatia Yanga manufaa ya goli moja na alama tatu, Bernard Morrison amesema kuwa kukataa kupiga penati kisheria ni kosa.

kukataa kupiga penati iliyoamuriwa na refa ni makosa MAKUBWA katika sheria na kanuni za mpira uwanjani. Ni sawa na kupigwa kadi nyekundu halafu ukagoma kutoka uwanjani. Kazi yetu uwanjani ni kucheza mpira na kumsikiliza mwamuzi aliyesomea kutafsiri kanuni na sheria”.

“Si kazi yetu kujua mwamuzi yupo sawa au laa, maana yeye ndio alienda darasani kwa kazi hiyo kama vile sisi tunavyovuja jasho viwanja vya mazoezi kuelewa namna ya kucheza . Cha msingi kila mmoja ajitahidi kuwa bora katika eneo la taaluma yake kama sisi tulivyoamua kuwa bora kutofungwa pia KUFUNGA PENATI KWA UBORA MZURI . “ Alisema Morrison

Baada ya Matokeo ya Jana Yanga wanaendelea kuongoza Ligi kwa kufikisha alama 20, na jumla ya michezo 45 bila ya kufungwa tangu Kocha wa timu hiyo Nasraddine Nabi ajiunge na Klbau hiyo April mwaka 2021.

Acha ujumbe