Winga wa zamani wa vilabu vya Simba na Yanga raia wa kimataifa wa Ghana Bernard Morrison yuko karibuni kujiunga na klabu ya Singida Fountain Gate.
Bosi wa klabu ya Singida Fountain Gate Japhet Makau amesema suala la Morrison kujiunga na klabu hiyo ni la muda kwakua wameshamalizana na mchezaji huyo, Huku akiwataka mashabiki wa klabu hiyo kutulia kwani mambo mazuri yanakuja.Klabu ya Singida Fountain Gate wanataka kufanya usajili mkubwa na wachezaji wenye ubora mkubwa kuelekea msimu ujao, kwani msimu ujao watakua wanashiriki michuano ya kimataifa ambayo ni kombe la shirikisho barani Afrika.
Super Ben ambaye ametua nchini Tanzania mwaka 2019 ni mcezaji mwenye uzoefu mkubwa ambapo ameshavitumikia vilabu viwili vikubwa vya Tanzania Simba na Yanga kwa vipindi tofauti akionesha uwezo mkubwa.Klabu ya Singida Fountain Gate wanaamini kumsajili Bernard Morrison inaweza kua sehemu ya maboresha ya kikosi chao, Kwani mchezaji huyo anapokua kwenye utimamu wake amekua akionesha uwezo mkubwa haswa kwenye michezo ya kimataifa.