MOSES PHIRI ATAMBA KUWAUA WAZAMBIA WENZAKE

MSHAMBULIAJI wa Simba, Moses Phiri amesema kuwa jambo ambalo lipo katika akili yake kwa sasa ni kuhakikisha kuwa wanaitoa timu ya Power Dynamos ili kufanikisha kutinga katika hatua inayofuata ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Moses Phiri atakuwa sehemu ya wachezaji wa Simba ambao watapambana na Power Dynamos ya kwao Zambia, ambapo kabla ya kutua Simba alikutana nao kwenye Ligi Kuu Zambia akiwa na Zanaco FC.moses phiriMoses Phiri alisema: “Kwa upande wangu akili zangu zote zipo katika mchezo wetu ujao wa kimataifa dhidi ya Power Dynamos.

“Ni timu ambayo naifahamu kwa kuwa mimi natokea Zambia, hautakuwa mchezo rahisi kwa kuwa kila timu ipo tayari kwa ajili ya kwenda hatua inayofuata.

“Binafsi kila kitu namuachia mwalimu kuhusu mimi kucheza au kutokucheza, kama nitapata nafasi ya kucheza basi nitajitahidi kuhakisha kuwa naipambania timu na tunapata matokeo mazuri,” alisema mchezaji huyo.

Acha ujumbe