Mshambuliaji wa Simba, Mosses Phiri amerejea uwanjani tena kwaajili ya mazoezi mepesi baada ya kukaa nje kwa wiki chache baada ya kupata kuumia kwenye mchezo wao wa Ligi dhidi ya Kagera Sugar uliopigwa tareehe 21 mwezi Desemba mwaka jana.

 

Mosses Phiri Arejea Uwanjani Tena

Mchezo huo ulimalizika kwa Simba kupata sare ya kufungana bao 1-1 huku Mosses akishindwa kuendelea na mchezo na kutolewa nje ya uwanja na ripoti zikaja baaadae kuwa atakuwa nje kwa muda wa siku kadhaa kwaajili ya kutibu jeraha alilopata.

Mshambuliaji huyo ndiye kinara wa mabao kwa upande wa vijana wa Juma Mgunda akiwa amepachika mabao 10 hadi sasa na akiwa ni wa pili baada ya kutanguliwa na Fiston Mayele mwenye mabao 14 Ligi Kuu.

Mosses Phiri Arejea Uwanjani Tena

Mazoezi hayo amabyo amenza kufanya yatamuweka fiti kwani mbio za ufungaji ni kali sana na bado ligi ni ngumu hivyo anahitajika arejee uwanjani mapema kabisa ili aongeze mabao na asipitwe na mshindani wake.

 

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa