Mfungaji Bora wa Ligi Kuu Bara msimu uliopita, George Mpole, ameibuka na kufunguka mengi makubwa yanayomuhusu mara baada ya kutoonekana kwa muda kikosini hapo.

Hiyo ikiwa siku ni siku chache zimepita tangu uongozi utoe taarifa za mshambuliaji huyo kutoweka kambini wakati timu hiyo ikiendelea kucheza michezo ya Ligi Kuu Bara.

Mpole, Mpole na Geita Gold Bado Ngoma Ngumu, Meridianbet

Mpole alisema hayupo katika timu hiyo, kutokana na kuuguza majeraha ambayo hivi sasa yanaendelea vizuri baada ya kutumia gharama zake mwenyewe.
Mpole alisema anawashukuru wale ambao wanajali uwezo wake, hasa Watanzania wanaompenda na kuona umuhimu wake kwa kumpigia simu wakimtakia heri akiwa anaendelea kujiuguza.

Aliongeza kuwa anashangazwa na uongozi wake kugomea kumlipa mshahara wake, kwa sababu ya kutokuwa na timu wakiwa wanafahamu kabisa yeye ni majeruhi na daktari ana taarifa zake.

“Viongozi wanaosema Mpole hayupo kwenye timu ndio haohao waliosema nisiwekewe mshahara kwa sababu sitaki kucheza, wakati kiuhalisia mimi nina majeraha.

“Mimi sijalipwa mshahara na timu ambayo nimepata majeraha nikiwa naipambania ili ipate matokeo ugenini, sijalipwa mshahara kwa sababu zisizo za msingi, daktari wa timu taarifa zangu anazo.

“Kuna wachezaji wengine wapo nyumbani zaidi ya miezi miwili na wanalipwa, lakini mimi nimeumia siku chache siwekewi mshahara.”

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa