MSHERY APATA MRITHI YANGA

MLINDA Mlango wa klabu ya Ihefu Abubakar Komeni amesajili na klabu ya Yanga kwa mkataba wa miaka miwili akiwa ni mrithi wa nyanda AbdulTwalib Mshery.

Komeni ambaye alikuwa amebakiza mkataba wa mwaka mmoja na Singida Black Stars, alipelekwa Ihefu kwa mkopo wa miezi sita dirisha dogo.msheryWiki iliyopitia Soka La Bongo tuliripoti kwamba kipa huyo aliuomba Uongozi wa klabu yake aondoke kutafuta changamoto mpya, ili kulinda kipaji chake na nafasi ya kuitwa timu ya taifa.

Mshery alijiunga na Yanga, Desemba 2021 hivyo ameitumikia timu hiyo kwa misimu mitatu yenye mafanikio kwa kutwaa mataji ya Ligi Kuu na Kombe la FA huku akiwa miongoni mwa wachezaji walioifikisha timu hiyo kucheza fainali Kombe la Shirikisho Afrika.

Chanzo cha kuaminika kutoka kwa rafiki yake wa karibu wa kipa huyo wa zamani wa Mtibwa Sugar na timu ya taifa ya vijana ya Serengeti Boys, kilifichua kuwa, Mshery amemaliza mkataba ndani ya Yanga na mpango wake ni kupata timu itakayompa nafasi ya kucheza mara kwa mara ili aweze kupata nafasi ya kuitumikia Taifa Stars.

“Mshery alisaini mkataba wa miaka mitatu ambayo tayari imeisha mwisho wa msimu huu sasa yupo timu ya taifa mambo yake ya kusaini mkataba timu nyingine bado hayajafanyika ila mpango wake ni kupata timu ambayo itamuakikishia nafasi ya kucheza,” kilisema chanzo hicho.

Juhudi za kumtafuta Mshery, ili kujua ukweli wa jambo hilo zilifanyika ili kuthibitisha ukweli wa jambo ambpo naye alikiri kweli mkataba wake na Yanga umeisha, lakini aligoma kuweka wazi ofa alizozipata hadi sasa ikiweka wazi kuwa muda ukifika kilakitu kitawekwa wazi.

“Ni kweli nimemaliza mkataba na Yanga baada ya msimu huu kuisha na nafurahi kuwa na misimu mitatu bora ndani ya timu hiyo licha ya changamoto mbalimbali nilizokutana nazo ikiwa ni pamoja na kukaa nje ya uwanja kwa muda kutokana na kusumbuliwa na majeraha,” alisema Mshery na kuongeza;

Acha ujumbe