Uongozi wa Mtibwa Sugar umebainisha kwamba utaweka kambi kwenye mashamba ya miwa yaliyopo Manungu, Morogoro kwa maandalizi ya msimu mpya.

Akizungumzia hilo, Ofisa Habari wa Mtibwa Sugar, Thobias Kifaru amesema kuwa kambi yao inatarajia kuanza Jumapili hii baada ya mapumziko ya wachezaji wao kumalizika.

Mtibwa, Mtibwa Hatuendi Popote Tutabaki Manungu, Meridianbet

“Wachezaji kwa sasa wapo mapumziko na kambi yetu tunatarajia kuiweka pale kwenye mashamba ya miwa Manungu, Morogoro na tutaanza rasmi Jumapili.

“Hatuhitaji kuweka kambi nje ya nchi kwasababu Manungu ni kama Ulaya hata Misri yenyewe haiwezi kufikia hadhi ya Mashamba ya miwa, kuna kila mahitaji yanayohitajika kwa timu lakini pia mazingira kiujumla yapo vizuri na yenye hadhi kubwa.

“Naamini kuwa timu haihitaji kuweka kambi nje ya nchi ili kufanya vizuri katika mashindano ya ndani, na ndio maana kwa upande wetu hatukuona umuhimu wa kufanya hivyo.

“Bado tunakamilisha mapendekezo ya benchi la ufundi kwa ajili ya kuweza kuwa na wachezaji wapya pamoja na wale ambao tulikuwa nao msimu uliopita.”

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa