BAADA ya ratiba ya ligi kuu kutangazwa rasmi leo, Uongozi wa Mtibwa Sugar umetamba kuwa hawauogopi mchezo wao wa kwanza dhidi ya Namungo na watafanya makubwa kwa msimu ujao.

Mchezo huo wa ligi kuu Bara kwa msimu wa 2022/23 unatarajiwa kupigwa Agosti 15 mwaka huu kwenye Uwanja wa Majaliwa, Lindi.

Mtibwa, Mtibwa Sugar Waahidi Kufanya Makubwa Msimu Huu, Meridianbet

Akizungumzia hilo Ofisa Habari wa Mtibwa Sugar, Thobias Kifaru amesema kwamba “Hatuna shaka na ratiba iliyopangwa kwani tumejiandaa vizuri kwa ajili ya kuhakikisha tunafanya vizuri.

“Tumeachana na nyota 19 ambao tulikuwa nao msimu uliopita waliopelekea kucheza playoffs kwa misimu iliyopita hivyo kwa sasa tuna jeshi kubwa la maangamizi.

“Tunatarajia kuonyesha ushindani mkubwa kwa msimu ujao hivyo niwatoe wasiwasi mashabiki wetu kwamba Mtibwa itakuwa ya moto sana msimu ujao na tuko vizuri sana, tutafanya makubwa msimu huu.”

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa