Mtibwa Sugar Uso kwa Uso Dhidi ya KMC Kombe la Shirikisho la Azam

Mchezo mwingine wa leo wa Kombe la Shirikisho la Azam hii leo ni kati ya Mtibwa Sugar dhidi ya KMC majira ya saa 10:00 jioni katika dimba la Manungu.

 

Mtibwa Sugar Uso kwa Uso Dhidi ya KMC Kombe la Shirikisho la Azam

Mtibwa kwenye ligi amecheza mechi zake 24, na kushinda mechi saba ,sare nane, na kapoteza tisa kati ya hizo huku akifanikiwa kujikusanyia pointi zake 29 mechi ya mwihso akipoteza. Na sasa yupo nafasi ya 9.

Huku KMC yeye akishikilia nafasi ya 13 ambayo sio nzuri kwa mwenendo anaoenda nao na mechi zimebaki chache kumaliza msimu huu. Walipa kodi wamepoteza mechi zao nne mfululizo kwenye ligi.

Mtibwa Sugar Uso kwa Uso Dhidi ya KMC Kombe la Shirikisho la Azam

Wameshinda mechi tano , sare nane na wamepoteza michezo 11 hadi sasa, akiwa na pointi 23 huku yeye na kibonde wa ligi wakiwa wamepishana alama 6 pekee hivyo asipoangali anaweza kuangukia pua msimu huu.

Sasa wanakutana kwenye Kombe la Azam huku mechi yao ya mwisho walivyokutana walitoshana nguvu. Je leo hii nani kuibuka mbabe?

 

 

Acha ujumbe