LIGI Kuu ya Vijana chini ya miaka 20 ilitamatika jana Jumapili kwenye uwanja wa Azam Complex na Mtibwa Sugar kufanikiwa kuwa mabingwa baada ya kuwachapa Mbeya Kwanza mabao 4-0.

Ushindi huo ukawafanya Mtibwa kuweka rekodi ya kutwaa ubingwa huo kwa misimu minne mfululizo na kuwa ndiyo wafalme wa ligi hiyo ya vijana na kuonyesha kuwa soka ndiko linakowekezwa.

Mtibwa Sugar, Mtibwa Sugar Bingwa wa Ligi Kuu Chini ya Miaka 20, Meridianbet

Mbali na ubingwa huo Mtibwa Sugar walifanikuwa kutwaa tuzo binafsi tatu, kocha bora ambaye alikuwa ni Awadh Juma, mchezaji bora akiwa Ladack Chadambi na kipa bora akiwa na Razack Shekimweri.

Kocha Awadh alisema kuwa mafanikio hayo yalitokana na uwekezaji wa kweli ambao wamekuwa wakiufanya kuanzia ngazi ya chini na wanaamini huo ni mwanga na matunda bora ya kazi yao ambayo wamekuwa wakifanya.

Azam FC walifanikiwa kuwa mshindi wa tatu baada ya kuwachapa Coastal Union kwa penalty 3-4 baada ya sare ya bao 1-1 kwenye muda wa kawaida. Geita Gold FC wao waliibuka kuwa timu yenye nidhamu.

Lakini pia kwa mara ya kwanza Tanzania ilishuhudia matumizi ya VAR kwenye ligi hiyo ambayo ilianza kutumika kwenye hatua ya nusu fainali.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa