Mlinda lango Andre krul (36) amejiunga na kikosi cha Mtibwa sugar kwa majaribio maalumu ya kuona kama anaweza kupata nafasi ya kucheza Ligi Kuu Bara.
Mlinda lango huyo raia wa Uholanzi ametua Turiani (Manungu) hivi kujaribu bahati yake huku pia akiwa na malengo ya kuweka historia ya kuwa mlinda lango aliyedakia klabu mbali mbali kutoka mabara yote duniani,
Misimu miwili ya nyuma Krul alishindwa kujiunga na Klabu ya Express ya Uganda kutokana na Janga la Covid 19.
Malengo ya krul ni kuhakikisha anacheza mabara yote duniani na katika mzunguko wake alisaliwa na bara la Afrika tu
Sasa yupo Mtibwa kwa majaribio ili kuona kama anaweza Kuendeleza historia yake hiyo.