Awali Mussa Mbisa alikuwa mchezaji wa klabu ya Coastal Union yenye makazi yake jijini kabla ya kusajiriwa na labu ya Tanzania Prison kwa mkataba wa miaka miwili
Akizungumzia hilo, Mbisa amesema kuwa “Nimefurahi sana kujiunga na Tanzania Prisons na ninaamini hapa nilipo ni sehemu sahihi kwangu kufanya vizuri zaidi kwa msimu ujao kwani ni timu inayoshiriki ligi kuu.
“Malengo yangu ni kufanya vizuri msimu ujao kuelekea malengo yangu kwani mipango yangu ni kuingia kwenye orodha ya makipa bora hata kuwa mshindi wa tuzo.”