Mzee Magori Awatuliza Simba Usajili.

KAZI imeanza na sasa heshima ya Simba inakwenda kurejea, ndiyo maneno ya mjumbe mpya wa Bodi ya Wakurugenzi wa klabu hiyo,Crescentius Magori baada ya kuteuliwa na mwenyekiti wa bodi, Mohammed Dewji ‘Mo’. Hajataka kupoteza muda, ameanza majukumu yake. Beti na Meridianbet utajirike haraka.

Mo Dewji alifanya uteuzi huo juzi Jumapili ambapo aliwachagua wajumbe ambao ni Mohamed Nassor, Salim Abdallah ‘Try Again’, Hussein Kita, Zulfikar Chando, Radhid Shangazi na Magori, watakaoongeza nguvu katika bodi hiyo.

Magori ni mtu wa maana kabisa na kazi yake ya usajili inafahamika na wengi, amewahi kushirikiana na Marehemu Hans Pope kuwasajili nyota kibao kama Mohammed Hussein, Chama, Rally Bwalya, Pape Sakho, Peter Banda, Medie Kagere, Mugalu, Thadeo Lwanga, Gerson Fraga Mkata umeme.

Unaambiwa kwamba mtaalum huyu wa masuala ya usajili, tayari yupo chimbo huko anasaka vipaji na watu wa kazi ili kuleta mabadiliko kwenye klabu ya Simba, baada ya misimu mitatu ya njaa na mateso kutoka kwa watani zao Yanga. Ulimwengu wa kubeti kirahisi umerahishwa na Meridianbet, kuwa wa kwanza kutimiza ndoto zako kupitia kasino.

Zambia ni moja ya kituo cha kwanza kufikiwa na Magori pamoja na timu yake kwenye usajili, taarifa za uhakika ni kwamba tayari wamemalizana na winga wa Power Dynamos Joshua Mutale.

Pia wanaiwinda saini ya kiungo wa Zesco Utd Kelvin Kapumbu ambaye uwezo wake unajulikana haswa kwenye Ligi ya Zambia. Amewahi kuwafunga Yanga kwenye mechi ya kirafiki.

Kasino inalipa sana, tembelea Meridianbet ubeti kirahisi.

Acha ujumbe