Kocha wa klabu ya Yanga Nasserdine Nabi amesema kua timu ambayo anaweza kuifundisha akiwa hapa nchini Tanzania ni klabu ya soka ya Yanga na sio timu nyingine yeyote.
Kocha Nabi ameyazungumza hayo kutokana na taarifa ambazo zinaendelea kusambaa juu ya kocha huyo kutaka kupewa kibarua cha kuinoa timu ya taifa ya Tanzania, Lakini kocha huyo amesema yeye yupo hapa nchini kwajili ya kuifundisha klabu ya Yanga.Timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars imekua haina kocha mkuu mpaka wakati huu wakati huohuo shirikisho la soka nchini Tanzania TFF limekua likitafuta kocha wa kuionoa timu hiyo, Hivo kocha huyo wa Yanga amekua akihusishwa na kupewa kibarua hicho.
Kocha Nabi amewaambia wanahabari kua ameona taarifa za yeye kuhusishwa na kupewa kibarua cha kuionoa timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars, Lakini yeye akisema kwasasa anafikiria kuhusu Yanga tu na ndo kazi iliyomfanya awepo hapa nchini mpaka pale atakapochukua uamuzi mwingine.Kocha Nabi amekua akifanya vizuri na klabu ya Yanga kwa msimu wa pili huku akiwaezesha kubeba ubingwa ligi kuu ya NBC, Huku akiwapeleka hatua ya makundi kombe la shirikisho kwa mara ya kwanza toka mwaka 2016 pamoja na wasifu mkubwa alionao kwenye soka la Afrika inaweza kua sababu ya kuhusishwa kuinoa Taifa Stars.