Kocha Mkuu wa Yanga Nasraddine Nabi amechukizwa na ushindi mdogo walioupata dhidi ya KMC wa bao 1-0 kwenye mchezo wa Ligi kuu ya NBC dimba la Benjamin Mkapa.
Kocha huyo aliwatupia lawama baadhi ya wachezaji wake, ambao amekuwa akiwapa nafasi ya kucheza lakini hawajitumi uwanjani na hiyo kuchangia timu ya Yanga kupata matokeo madogo na kucheza kwa kiwango kidogo.“Leo tumecheza mpira usio kuwa wa kawaida kwetu na matokeo madogo, lakini inashangaza sana na kuchukiza unawapa nafasi baadhi ya wachezaji ambao hawatimizi majukumu yao, na hii ni tatizo la msimu mzima kuna wachezaji hapa tangu wasajiliwe hawabadiliki” Kocha Nabi alizungumza baada ya mchezo kumalizika.
Kwa upande wa Kocha wa KMC Thiery Hitimana alisema kwamba wamefungwa kutokana na kupoteza umakini ndani ya uwanja.Matokeo haya yanaifanya Yanga kuongoza Ligi kuu kwa utofauti wa pointi 8, huku akifukuziwa na watani zao Simba aliyetoka kulazimishwa sare na Azam FC jana.