Taarifa kutoka Afrika kusini zimethibitisha kuwa Hakuna Uwezekano tena wa Kocha Nasreddine Nabi kujiunga na klab ya Kaizer Chiefs na tayari Muwakilishi wa kocha huyo aliyekuwa Afrika Kusini tayari ameondoka siku ya leo.
Inadaiwa Nabi alipendekeza aingie na benchi lake la Ufundi klabuni hapo kitu ambacho Uongozi wa klab ya Kaiezer Chiefs haukuliafiki kwakuwa tayari walikuwa na watu wao wa kwenye benchi la Ufundi,Imefahamika Uongozi wa klab hiyo Umekubaliana kusaka Kocha Mwingine atakaye kubaliana na Matakwa yao.Mwandishi wa FARSPORT kutoka Afrika Kusini Mthokozisi Dube amesema hakuna uwezakano wa kocha huyo kwa sasa kuisimamia Kaizer na hata viongozi bado hawataki kuweka wazi jambo hilo