Kocha Mkuu wa Yanga, Nassredine Nabi amefunguka kuwa sababu ya kuruhusu mabao ya kushambulia kwa kushtukiza ni mabeki wake kujisahau.

Nabi aliongea hayo jana jumapili baada ya kumalizika kwa mchezo wa ligi dhidi ya Simba ambapo timu hizo zilitoka sare ya bao 1-1.

Yanga, Nabi Aweka Wazi siri ya Yanga Kupata Sare, Meridianbet

Nabi alisema kuwa: “Ilikuwa mechi ya wazi kuliko nyingine kwani kila mmoja alikuwa na nafasi ya kupata ushindi.

“Naweza kusema vipindi viwili viligawanywa, Simba walikuwa bora kipindi cha kwanza lakini sisi tulikuwa bora kipindi cha pili ila kuna nafasi tulizipata tukashindwa kuzitumia.

“Kila mtu amestahili kile alichokipata, tumekuwa tukifungwa magoli ya mashambulizi ya kushtukiza na hii inatokana na wale ambao wanaenda mbele kushambulia wanasahau kurudi kukaba lakini tunarudi mazoezini kwa ajili ya kulirekebisha hilo.”

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa