BAADA ya kupata majeraha ya mguu, kiungo mshambuliaji wa Azam FC, Iddy Nado tayari ameanza mazoezi kwa ajili ya kurejea tena uwanjani.

Nado alipata majeraha ya goti ambayo yalimlazimu kwenda nje ya nchi kwa ajili ya kupatiwa matibabu zaidi.

Akizungumza kurejea kwake uwanjani, Ofisa Habari wa Azam FC, Thabit Zakaria ‘Zaka zakazi’ amesema kuwa nyota huyo tayari ameanza mazoezi binafsi.

“Nado tayari ameanza mazoezi binafsi kwani mwezi wa nane anatarajiwa kuanza mazoezi na timu na baada ya hapo atarejea rasmi uwanjani.” -Zaka zakazi

Nado Aanza Tizi Azam

 

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa