Namungo Apasuka Nyumbani Kwake

Klabu ya Namungo FC imepoteza mchezo wake hapo jana wlaiokuwa wakicheza dhidi ya Tanzania Prisons kwenye mchezo wa ligi kuu ya Tanzania Bara katika dimba la Majaliwa majira ya saa 1 usiku.

 

Namungo Apasuka Nyumbani Kwake

Namungo alipoteza kwa mabao 2-3 ambapo kwa upande wao mabao yalitupiwa kimyani na Hassan Kabunda na Lusajo, huku kwa upande wa Prisons wao mabao yao yaliwekwa kambani na Bangula, Jeremia pamoja na Balua.

Baada ya ushindi huo, sasa Tanzania Prisons ambao walikuwa wakiuhitaji ushindi huo wapo nafasi ya 13 kwenye msimamo wa ligi kuu huku wakiwa na pointi zao 25 ambazo bado pia hazitoshi kuwabakiza kwenye ligi.

Namungo Apasuka Nyumbani Kwake

Namungo wao baada ya kupoteza mechi hiyo wanashikilia nafasi ya saba, huku wakiwa sawa pointi na aliyepo nafasi ya sita kwenye ligi .

 

 

Acha ujumbe