Namungo Dhidi ya Geita Gold Kumenyana Leo

Ligi kuu ya NBC kuendelea hii leo kwa mchezo mmoja ambapo Namungo FC itakiwasha dhidi ya Geita Gold kutoka mkoani Geita.

 

Namungo Dhidi ya Geita Gold Kumenyana Leo

Mechi hiyo inatarajiwa kupigwa majira ya saa 1:00 usiku katika kiwanja cha Majaliwa huku kila timu ikihitaji pointi tatu ili kuendelea kujiweka kwenye nafasi nzuri kwenye msimamo wa ligi.

Namungo anashikilia nafasi ya 8 kwenye msimamo wa ligi wakiwa wamecheza mechi zao 23, ushindi mara nane, sare tano na wamepoteza mara kumi hadi sasa huku wakiwa na pointi zao 29.

Wakati kwa upande wa Geita Gold ya Minziro wao wanashikilia nafasi ya tano, wakiwa wameshinda mechi zao nane, sare kumi na kupoteza mara tano wakikusanya alama zao 34 kwenye msimamo.

Namungo Dhidi ya Geita Gold Kumenyana Leo

Vijana wa Lindi wametoka kupoteza mechi mbili mfululizo, huku kwa upande wa Wachimba dhahabu wao wameshinda mechi mbili mfululizo. ODDS KUBWA unazipata Meridianbet pekee ingia na ucheze.

Mechi ya mwisho kukutana timu hizi mbili, wachimba madini waliondoka na ushindi wakiw anyumbani kwao. Je leo hii ni nafasi nzuri ya Wauuaji wa Kusini kulipa kisasi?

 

Acha ujumbe