Nusu fainali ya pili ya Mapinduzi Cup ilipigwa jana ambapo ilishuhudiwa kuwa na ugumu wa kiasi chake baada ya Namungo kushindwa kufurukuta dhidi ya Mlandege na kusababisha timu hizo kutoka sare.
Namungo imeshindwa kwenda hatua ya fainali ya Mapinduzi Cup baada ya kuondolewa kwenye hatua ya matuta kwa 5-4. Timu hiyo kutoka Lindi ilishindwa kulinda bao lao la mapema walilolifunga kupitia kwa mchezaji wao Ibrahi Mkoko.
Bao lilisawazishwa ndani ya dakika 45 za kabla ya kipyenga cha mwamuzi kumalizika cha mapumziko na walivyorejea kipindi cha pili hakuna aliyeweza kuona lango lake na mwisho ikawabidi waende hatua ya penalti.
Mlandege ndio wakaibuka vinara baada ya kuwashinda Wauuaji wa Kusini kwa mikwaju ya penalti 5-4 na timu hiyo kusonga mbele hatua ya fainali kukiwasha dhidi ya Singida Big Stars.