Ligi kuu ya NBC kuendelea hii leo kwa michezo miwili, mchezo mojawapo ni kati ya KMC dhidi ya Namungo ya Mkoani Lindi.
KMC wametoka kupata sare mechi yao iliyopita, huku Namungo wao wakitoka kupoteza mchezo wao wa mwisho kwenye ligi, huku wakiwa tayari wameshacheza michezo 20 mpaka sasa.
Kwenye hiyo michezo waliyocheza, wapo nafasi ya sita wameshinda michezo saba wakitoa sare tano na kupoteza michezo nane, na kujikusanyia pointi zao 26.
Wakati Wanakino Boys ya Thierry Hitimana wao wana hali isiyoridhisha kwenye Ligi kwani wao nafasi ya 10, baada ya michezo 20, wakishinda michezo mitano sare nane na kupoteza mara saba na kupata alama 23.
Mechi nne za mwisho kukutana timu hizi mbili wametoka sare, hakuna aliyekuwa mbabe. Leo wanakutana tena nani kuondoka kifua mbele.