Nasradine Nabi Atoa Angalizo kwa Mnyama, Kisa Yanga

Nasredine Nabi kocha Mkuu  wa Kaizer Chief ameweka wazi kuwa Yanga ina mabadiliko makubwa na chochote kinaweza kumkuta yoyote msimu ujao. Jisajili hapa kuwa wa kwanza kushinda Mamilioni ya Meridianbet kila siku.

Nabi ambaye ni kocha wa zamani wa Yanga, amekiri kwa uchungu kwamba kilichoomuumiza zaidi kwenye mechi ya juzi ni ukubwa wa kipigo ilichopata timu yake; “lakini tulistahili.”

Yanga tayari ipo nchini na kombe lao la Toyota walilobeba nchini Afrika Kusini ilipoweka Kambi ya muda ya maandalizi ikiichapa Kaizer Chiefs mabao 4-0.

Nabi ambaye hiyo ilikuwa mechi yake ya kwanza kubwa ya kirafiki baada ya kutoka kambini Morocco,alisema hata hivyo Yanga imebadilika na kuwapa shida ya kupoteza mpira kwa haraka wakati wanaumiliki iliyowalazimu wachezaji wake wengi vijana kushindwa kuhimili presha hiyo.

Beti na Meridianbet kwa ushindi mkubwa na odds kubwa, Ligi  zinakaribia kuanza,  usije kupishana na gari la Mshahara.

Aliongeza kuwa kitu ambacho imekutana nacho timu yake kinaweza kuikumba timu yoyote ndani na nje ya Tanzania msimu ujao ambayo haijajiandaa sawasawa kukutana na mbinu za namna hiyo za timu inayoweka presha kubwa kwa wapinzani wanapokuwa na mpira.

“Timu yetu ina wachezaji wadogo kidogo ambao hawakuwa tayari kukutana na ugumu wa namna ile, ukiangalia unaona namna ambavyo Yanga ilipokuwa haina mpira iliweka presha kubwa kwetu na vijana kujikuta wanafanya makosa makubwa,”alisema Nabi ambaye ambaye ana uraia wa Tunisia.

“Kuna mabao ambayo mliyaona ni kama yalikuwa zawadi kwao,lakini nadhani tumejifunza nadhani kilichotokea kwetu kinaweza kuikuta timu yoyote ambayo haikujiandaa sawasawa kukutana na mbinu za namna ile,”alisisitiza Kocha ambaye alikiri kwamba bado ana muda wa kuisuka timu yake.

Michezo ya Kasino na Sloti ni machimbo yanayotoa pesa kirahisi. Cheza kasino hapa.

Acha ujumbe