TIMU ya Taifa ya Tanzania chini ya miaka 23 ‘Ngorongoro Heroes’ imefanikiwa kuiondoa Sudan Kusini kwenye michuano ya kufuzu AFCON baada ya kutoka sare ya mabao 3-3.

Mchezo huo wa kutafuta nafasi ya kufuzu AFCON ulipigwa jana jumatatu kwenye Uwanja wa Huye uliopo nchini Rwanda.

 

Ngorongoro Heroes yaitoa Sudan Kusini AFCON

Mabao ya Tanzania yalifungwa na Abdul Sopu, Ally Msengi na Kelvin John ambayo yaliipeleka Tanzania katika hatua inayofuata.

Kwenye mchezo wa kwanza uliopigwa katika Uwanja wa Azam Complex Chamazi, Dar ulimalizika wa suluhu ya bila kufungana ambapo Tanzania imevuka baada ya kupata mabao ya ugenini.

 

Ngorongoro Heroes yaitoa Sudan Kusini AFCON

Katika hatua inayofuata Ngorongoro Heroes watakutana na Nigeria kwa ajili ya kutafuta nafasi hiyo ya kushiriki michuano ya AFCON.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa