Nickson Kibabage Anukia Singida Big Stars

Nahodha wa klabu ya Mtibwa Sugar kutoka mkoani Morogoro Nickson Kibabage inaelezwa ananukia kwa walima alizeti kutoka Singida klabu ya Singida Big Stars.

Beki huyo wa zamani wa klabu ya KMC ya jijini Dar-es-salam amewekewa ofa nzuri na klabu ya Singida Big Stars na siku sio nyingi beki huyo wa kushoto atamwaga wino kuwatumikia walima alizeti hao kutoka mkoani Singida.nickson kibabageTaarifa za ndani zinaeleza Nickson Kibabage amewaaga wachezaji wenzake ndani ya klabu ya Mtibwa Sugar akiwa tayari kwa safari ya kuelekea klabu ya Singida Big Stars, Beki huyo atakumbukwa klabuni hapo kutokana na ubora wake aliouonesha ndani ya klabu hiyo kwa kipindi kifupi alichokuepo.

Beki huyo mnyumbulifu pia inaelezwa alikua kwenye rada za wekundu wa msimbazi klabu ya Simba ambao walikua wamepanga kumsajili beki huyo mwishoni mwa msimu, Lakini klabu ya Singida wao wamekuja na ofa nzuri mapema na imedfanikiw kumshawishi Nickson Kibabage.

Acha ujumbe