Ntibazonkiza Apewa Thank You Simba

Aliyekua kiungo mshambuliaji wa klabu ya Simba raia wa kimataifa wa Burundi Saidoo Ntibazonkiza amepewa kwaheri ndani ya klabu ya Simba ambapo amemaliza mkataba wake na wameamua kutomuongezea.

Ntibazonkiza ambaye alijiunga na Simba mwezi Januari mwaka 2023 kwenye dirisha dogo amedumu ndani ya klabu hiyo kwa mwaka mmoja na nusu, Ambapo klabu ya Simba imeamua kumalizana na kiungo huyo baada ya makubaliano ya pande zote mbili ya kutomuongezea mkataba.ntibazonkizaKiungo huyo wa kimataifa wa Burundi alipojiunga na klabu ya Simba alikua moja ya wachezaji tegemezi klabuni hapo ambapo mpaka alifanikiwa kumaliza kama mfungaji bora kwenye msimu wa mwaka 2022/23, Lakini msimu uliomalizika mchezaji huyo alionekana kuporomoka ubora na kufikia hatua ya klabu ya Simba kutomuongezea mkataba.

Klabu ya Simba ipo kwenye mchakato wa kupiga fagio wachezaji ambao wanaona hawataweza kuipeleka mbele klabu hiyo, Hivo moja ya wachezaji ambao wameonekana hawana uwezo mkubwa wa kuisaidia timu hiyo siku za mbeleni ni Saidoo Ntibazonkiza.

Acha ujumbe