Nyota mpya wa Simba, Saido Ntibazonkiza baada ya kujiunga amekabidhiwa namba kubwa ya jezi ambayo ni 39.
Saido alitambulishwa hivi karibuni akitokea Geita Gold ambapo alidumu kwa nusu msimu.

Baada ya kutambulishwa, Saido alijiunga fasta kwenye kikosi hicho kinachonolewa na Kocha Mkuu, Juma Mgunda kilichokuwa Jijini Mwanza.
Nyota huyo amepewa jezi namba 39 jambo ambalo wengi hawakutarajia kutokana na ukubwa wa jina la mchezaji huyo.


