MCHEZAJI wa Simba Agustine Okrah ambaye ni raia wa Ghana, ametumia mtandao wake wa kijamii kufafanua suala la yeye kushindwa kutengeneza nafasi kwa wachezaji wenzake kwenye mechi ya watani wa jadi Yanga Vs Simba ambapo matokeo ya mwisho yalikuwa ni sare ya 1-1.

 

Okrah Aomba Msamaha Mashabiki Zake.

Okrah alisema kuwa “Kila ninachokifanya nafanya kwaajili ya timu, Acha tusahau yaliyopita tutazame kwenye mchezo unaofuatia”

Hii imetokana na Mashabiki wengi wa timu ya Simba kupeleka shutuma na malalamiko yao kwa mchezaji huyo, kuwa alikuwa mchoyo wa kutoa pasi kwa wachezaji wenzake kama vile Clatous Chama na Moses Phiri ambao walikuwa kwenye nafasi nzuri zaidi ya kufunga, ila yeye akachagua kufunga kwa kucurve ila haikuwa sehemu ya hesabu sahihi kwake.

Katika mchezo huo Simba ndiyo ilitanguilia kupata goli kupitia kwa mchezaji Agustine Okrah katika dakika ya 15 ya mchezo, kabla ya bao la kusawazisha kwa Yanga lililofungwa na Stephen Aziz KI dakika 2 za nyongeza kipindi cha kwanza.

Hata hivyo baada ya posti hiyo, mashabiki walimjibu mchezaji huyo huku wengi wakionekana kumshauri zaidi na kumtia moyo.

Okrah Aomba Msamaha Mashabiki Zake. okrah, Okrah Aomba Msamaha Mashabiki Zake., Meridianbet okrah, Okrah Aomba Msamaha Mashabiki Zake., Meridianbet

 

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa