Okrah Atemwa Yanga, Injinia Hersi Kushusha Vyuma

BECHEM United ya Ghana imepanga kumrejesha nyumbani winga wa Yanga, Augustine Okrah aliyeonekanakukosa nafasi ya kucheza chini ya kocha Miguel Gamondi. Imeripotiwa Waghana wamefungua milango kwa winga huyo aliyefanya vizuri akiwa na timu hiyo kabla ya kurejea Tanzania wakati wa dirisha dogo, awali aliichezea Simba. Ushindi wa pesa yako upo Meridianbet pekee bashiri mubashara kwa ushindi mkubwa.

Okrah Magic alisajiliwa na Yanga kipindi cha dirisha dogo, na kutambulishwa kwa staili ya aina yake akiwa kafunikwa kitu maalum na kuoneshwa katika uwanja wa New Amaan Zanzibar.

Amehudumu katika ya Yanga kwa miezi 6 tu, na mechi alizocheza akiwa na klabu ya wananchi Yanga, takribani mechi 4 za Ligi na moja ya mashindano ya Kombe la Mapinduzi. Kwa kujisajili Meridianbet,  unajiweka karibu zaidi na utajiri.

Kwa taarifa za ndani ya Yanga zinasema kwamba, nyota huyo Raia wa Ghana hatukuwa sehemu ya kikosi cha timu hiyo kwa msimu ujao 2024/25, hivyo taratibu za kumpa mkono wa kwaheri zinafanyika.

Dirisha la usajili wa Ligi kuu Tanzania Bara na Ligi ya Championship linafunguliwa tarehe 15 Juni, huku kila timu ikiwa inasubiri kwa hamu usajili mpya.

Yanga atacheza kimataifa msimu ujao, Ligi ya Mabingwa Afrika kwa hiyo anatakiwa kufanya usajili wa maana ili kukipa makali kikosi chake, Rais wa Yanga Injinia Hersi hivi karibuni alinukuliwa akisema “tutafanya usajili wa maana wenye kuleta ushindani kwenye kikosi chetu, wachezaji muhimu hatuwezi kuwaacha”

Acha ujumbe