OKRAH KUTAMBULISHWA LEO ZANZIBAR

NYOTA Agustino Okrah ambaye amecheza ndani ya kikosi cha Simba kabla ya kukutana na mkono wa kwaheri yupo Visiwani Zanzibar na leo YANGA wanayarajia kumtangaza rasmi.

Inaelezwa Yanga wameingia kandarasi ya miaka miwili na nyota huyo Okrah ambaye alikuja Simba Msimu uliopita akiwa amebeba matumaini makubwa ya kufanya vizuri.OKRAHOfisa Habari wa Yanga Ali Kamwe alithibitisha uwepo wa Okrah Zanzibar Kwa Lugha ya mafumbo, akimuita mgeni Mwenyeji.

“Mgeni mwenyeji yupo Zanzibar na kesho (Leo) tutamtambulisha Rasmi Kwa Mashabiki Ili wamuone.

 

OKRAH“Ni mchezaji Mzuri ambaye kwetu tunaamini anakuja kuongeza kitu kwenye timu yetu,” alisema Kamwe.

Acha ujumbe