Kiungo wa klabu ya soka ya Simba Nelson Okwa ameejea nchini akitokea kwao nchini Nigeria ambapo alienda kupatiwa matibabu baada ya kupata majeraha.

Kiungo huyo alipata majeraha alipata majeraha ya nyama za paja kabla ya mchezo wa ligi kuu ya NBC dhidi ya klabu ya Azam Fc na kumfanya kurudi nchini kwao kwenda kupatiwa matibabu na hivo kurejea siku ya jana.okwaKiungo Okwa ambaye alisajiliwa dirisha lililopita akitokea klabu ya Rivers Ubited ya nchini Nigeria ambapo alikua anaonesha ubora mkubwa tofauti na ndani ya klabu ya Simba ambapo mpaka sasa hajafanikiwa kuonesha cheche zozote.

Kiungo Nelson Okwa amekua akisumbuliwa na majeraha ya mara kwa mara tangu ajiunge na klabu ya Simba kwenye dirisha lililopita kitu kinachomfanya kukosa nafasi ya kudumu ndani ya kikosi cha wekundu wa msimbazi.okwaTetesi zinaeleza Simba wana mpango wa kupitisha panga kwenye kikosi chake mwezi Januari na kusajili wachezaji wapya ambapo inaelezwa miongoni mwa wachezaji ambao wamepangwa kuachwa ili wengine waingie ni kiungo huyo wa kmataifa wa Nigeria.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa