Okwa Nitawafunga Yanga

Okwa ambaye amejiunga na Simba kutokea ndani ya kikosi cha Rivers United ya Nigeria juzi Jumatatu aliichezea Simba mchezo wa kwanza dhidi ya ST George ya Ethiopia ambapo aliingia kipindi cha pili na kufunga bao dakika ya 55, ambalo lilikuwa la pili kwenye ushindi wa mabao 2-0 walioupata Simba katika mchezo huo.

Akiwa na Rivers United, Okwa aliwahi kucheza na Yanga katika mchezo wa mtoano wa Ligi ya Mabingwa Afrika msimu uliopita ambapo Yanga walipoteza michezo yote miwili kwa bao 1-0.

Okwa alisema: “Ni jambo kubwa kwangu kufunga bao katika mchezo wangu wa kwanza nikiwa na Simba, nimeshangazwa sana na upendo mkubwa ambao nimeonyeshwa na wachezaji wenzangu na mashabiki kwa ujumla kulinganishja na kwetu Nigeria.

“Nilichoonyesha leo ni mfano tu wa kile ambacho nitakuja kukifanya kwenye ligi na mashindano mbalimbali msimu ujao, natarajia kufanya makubwa zaidi kwa ajili ya kuisaidia Simba kushinda makombe msimu ujao.

“Kuhusu Yanga nawajua vizuri kwa kuwa niliwahi kucheza dhidi yao na najua wana kikosi bora, lakini sina presha na kama ambavyo nimesema nimekuja Simba kushinda mataji hivyo nitajituma kuhakikisha tunashinda Jumamosi.”

Acha ujumbe