Kaimu Kocha Mkuu wa Azam FC Kally Ongala amefunguka kuwa mshambuliaji wa timu hiyo Prince Dube raia wa Zimbabwe ni moja kati ya wachezaji bora kwenye kikosi hicho na hata ligi ya Tanzania.

Ongala alisema, wengi wanasahau uhatari wa Dube kutokana na kutoonekana uwanjani kwenye baadhi ya mechi kutokana na majeraha ya mara kwa mara na kama akiwa fiti kwa asilimia 100 mchezaji huyo hufanya mambo makubwa sana akiwa uwanjani.

Ongala, Ongala: Yule Dube Siyo Mtu wa Kawaida, Meridianbet

“Dube ni mchezaji bora kwenye kikosi chetu, ni mchezaji ambaye atakupa unachokihitaji uwanjani kwa asilimia 100 kama akiwa fiti. Anaweza asifunge, lakini akatengeneza pasi ya goli au akatengeneza mpango wa goli kupatikana.

 

“Kitu pekee ambacho kinawasaulisha watu ni majeraha. Nafikiri watu wameona alichofanya kwenye mechi yetu na Simba akifunga goli la ushindi kwa timu yetu, il ani mchezaji mzuri sana.”

Alisema Ongala.

Ongala amevuna alama nne kwenye mechi mbili za Simba na Yanga ambazo alisimama kwenye benchi la Azam. Alianza kwa sare ya bao 1-1 na Yanga na sasa ushindi wa bao 1-0 mbele ya Simba na amefanikiwa kuvunja mwiko wa miaka mitano ya kutowafunga Simba.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa