Pambano la Mfaume Mfaume na Iddy Pialali lasitishwa katika raundi ya kwanza ya mchezo kutokana na na Pialali kupata jeraha ambalo lilimfanya ashindwe kuendelea kupigana.
Licha ya kusubiriwa kwa hamu na mashabiki wengi wa mchezo wa masumbwi, pambano la wawili hao limesitishwa kutokana na Iddy Pialali kupata majeraha baada ya kugongana na mpinzani wake
Pialali alionekana akilalamika, baada ya mwamuzi kusimamisha pambano hilo ikabainika alichanika karibu na jicho, akawa anavuja damu kwa wingi hivyo mwamuzi aliona haina haja ya pambano hilo kuendelea.
Kutokana na hali hiyo, pambano hilo lililofanyika Ukumbi wa AICC Mkoani Arusha halikuwa na mshindi na kushauriwa promota apange marudio baina ya mabondia hao ili apatikane mshindi.




